Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Vikundi vya Wanawake vya Indonesia na vile vya Zanzibar kuanzisha ushirikiano
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein amesisitiza haja ya kuwepo kwa mashirikianao kati ya vikundi vya wanawake vya Indonesia na vile vya Zanzibar kwa lengo la kuongeza kasi katika juhudi zao za kujileta maendeleo.Mama Shein aliyasema hayo wakati alipotembelea viwanda vidogo vidogo pamoja na vikundi vya akina mama vinavyojishughulisha na ujasiriamali vilivyo mjini Jakarta. Alimpongeza Makamo wa Rais wa Indonesia Muhammad Jussuf Kalla kwa mwaliko alioutoa kwa Rais wa Zanzibar na kuwapongeza wananchi wote wa Indonesia naa viongozi wao kwa mapokezi makubwa waliyoyatoa kwa Rais Dk. Shein pamoja na ujumbe wake aliofatana nao katika ziara hiyo.Mama Shein alionesha furaha yake kwa kutembelea viwanda vidogo vidogo na sehemu za wajisiriamali ambapo alisema kuwa ziara hiyo inakwenda sambamba na shughuli anazofanya yeye na viongozi mbali mbali wanawake wa Zanzibar katika kuhamasisha suala zima la uwezeshaji wa wanawake na shughuli zao za ujasiriamali. Katika hotuba yake, Mama Shein alieleza juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwawezesha wanawake ikiwa ni pamoja na kuvihamasisha vikundi vya ujasiriamali sambamba na kuimarisha hali na maendeleo ya watoto.Mama Shein alieleza kwamba idadi ya wanawake wa Zanzibar ni zaidi ya asilimia 50 ya watu wake ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua kwamba idadi hiyo kubwa ya wanawake haiwezi kuachwa nyuma katika kuleta maendeleo ya haraka nchini humo. Alieleza kwamba miongoni mwa juhudi anazozichukua pamoja na akina mama wa Zanzibar ni kuhamasisha maendeleo ikiwemo elimu kwa wanawake, maendeleo ya afya kwa akina mama na watoto pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.Aliongeza kuwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo yeye kwa upande wake amekuwa akiziunga mkono katika kuimarisha afya ya mama na watoto zimesaidia sana kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama na watoto. Alisema kuwa ziara hiyo aliyoifaya itampa elimu na maarifa mapya katika utekelezaji wa shughuli hizo wanazozifanya akinamama na kuchukua fursa hiyo kuwapongeza wanawake wa Indonesia kwa mwamko mkumbwa walionao wa kujitafutia maendeleo yao wenyewe.Aidha, aliipongeza Serikali ya Indonesia kwa juhudi kubwa ilizochukua kwa kuimarisha haki za wanawake na watoto pamoja na kuunga mkono utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali za maendeleo wanazozifanya. Mama Shein alifahamisha kwamba unapomsaidia mwanamke ni rahisi sana mchango wake kwenda moja kwa moja kwa jamii kwa upana zaidi kwani wanawake wanajukumu kubwa sana katika shughuli za familia na za zile za kijamii.Hivyo, Mama Shein alipendekeza haja ya kuwepo mashirikiano ya karibu kati ya vikundi vya ujasiriamali vya akina mama wa Indonesia na vile vya Zanzibar na kueleza kuwa hatua hiyo itaimarisha utekelezaji wa shughuli mbali mbali wanazozifanya huku akisisitiza haja ya kutumia uhusiano uliopo kupitia Serikali zao ili kuimarisha mashirikiano hayo. Pia, Mama Shein alisisitiza juu ya umuhimu wa kuanzisha utaratibu utakaowawezesha akina mama wa Indonesia na wale wa Zanzibar kutembeleana na kubadilishana uzoefu kama ni msingi muhimu wa kupata mafanikio kwa shughuli zao kujiletea maendeleo wanazozifanya.Mama Shein alivipongeza vikundi hivyo kwa kuandaa shughuli hiyo ambayo imeonesha jinsi walivyokomaa katika kujiletea maendeleo na kuhakikisha nafasi ya mwanamke inathaminiwa. Nae Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujasiriamali na Ushirika ya Indonesia Emila Suhaimi alitoa pongezi kwa Mama Shein kwa hatua yake ya kuvitembelea vikundi vyao hivyo na kutumia fursa ya kumuonesha shughuli zao mbali mbali wanazozifanya.Alieleza kuwa hatua ya Mama Sheuin ya kuwatembelea akina mama hao inaonesha wazi jinsi anavyowathamini wajasiriamali na akina mama wote kwa jumla ambapo pia, imezidi kujenga uhusiano na ushirikiano mwema uliopo kati ya Indonesia na Zanzibar. Aliongeza kuwa miongoni mwa mikakati ya Serikali ni pamoja na kuhakikisha wanaviwekea mazingira mazuri vikundi vya akinamama wajasiriamali ili wapate fursa nzuri katika kujifunza biashara, kuuza na kuzitangaza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.Aidha, Suhaimi alieleza kuwa kuna vikundi zaidi ya 4,000 ambapo kila kikundi kina bidhaa zake wanazoziuza ndani ya jengo hilo ambalo wamepewa maalum na serikali kwa azma ya kufanya shughuli zao hizo jambo ambalo limesaidia kuwaweka pamoja akina mama. Wakati huo huo, Mama Shein alitembelea katika jingo la Alun-alun ambalo akina mama wamekuwa wakiuza bidhaa zao mbali mbali.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo