Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Suza kuanzisha uhusiano na ushirikiano na Chuo cha Utalii cha Bali
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa fursa maalum kwa uongozi wa Chuo cha Utalii cha Bali kuanzisha uhusiano na ushirikiano kati ya Chuo hicho na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).Akizungumza na uongozi wa Chuo cha Utalii cha Bali huko katika ukumbi wa Chuo hicho, Rais Dk. Shein alisema kuwa kutokana na chuo hicho kushabihiana kati ya kada zake na za utalii na kada inayotolewa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya utalii Zanzibar. Alisema kuwa chuo hicho kimepata mafanikio makubwa ambayo yanaweza kusaidia katika mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha sekta ya utalii kwa kutoa mafunzo, kubadilishana uzoefu na utaalamu pamoja na kutembeleana kwa lengo la kujifunza baina ya chuo hicho na chuo kikuu cha SUZA.Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuueleza uongozi huo wa Chuo hicho cha Utalii azma pamoja na mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kukiendeleza zaidi chuo chake cha Maendeleo ya Utalii. Alieleza kuwa kwa hivi sasa chuo hicho kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza kada za masomo pamoja na kuanzisha Shahada ya Kwanza inayohusiana na masuala ya uatlii.Aidha, Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa ziara yake hiyo nchini Indonesia mbali ya kulenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo pia, ina lengo la kujivunza jinsi ya nchi hiyo inavyoendesha sekta ya utalii ambayo imeleta mafanikio makubwa kwa Zanzibar na Indonesia hasa katika kisiwa hicho cha Bali ambacho kinatajika kwa utalii duniani. Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein aliuhakikishia uongozi huo kuwa mashirikiano ya pamoja yatahakikishwa yanaimarishwa kati ya Chuo hicho na chuo kikuu cha SUZA ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha pamoja viongozi wa vyuo hivyo ili kuadiliana kwa mpamoja juu ya kuimarisha mashirikiano hayo.Rais Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kuualika uongozi wa chuo hicho kuitembelea Zanzibar pamoja na kukitembelea Chuo Kikuu cha SUZA. Nae Mkurugenzi Mkuu wa Chuo hicho Dk. Dewa Gede Ngurah Byomantara alimpongeza Rais Dk. Shein kwa kutembelea chuo hicho ambacho kimepata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Indonesia katika kufundisha kada ya Utalii. Mkuu huyo wa Chuo hicho cha Utalii alimueleza Rais Dk. Shein namna ya chuo hicho kinavyotoa mafunzo ya utalii kuanzia cheti hadi Shahada za juu katika fani mbali mbali za utalii pamoja na mafunzo ya muda mfupi.Katika maelezo yake, Mkuu huyo wa Chuo alimpongeza Rais Dk. Shein kwa kutoa fursa hiyo ya mashirikiano kati ya chuo hicho na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), na kueleza kuwa hatua hiyo itafungua ukurasa mpya wa mashirikiano katika mafunzo ya utalii kati ya pande mbili hizo. Wakati huo huo, Rais Dk. Shein alitembelea eneo la utamaduni la Garuda Waisnu Kencana na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Biashara Arifin Tirta Wijata kuhusiana na alama mbali mbali za utamaduni zilizopo katika eneo hilo ambalo ni maarufu mjini Bali. Katika maelezo yake Mkurugenzi huyo alimueleza Rais Dk. Shein kuwa alama zilizopo katika eneo hilo zimekuwa ni kivutio kikubwa cha watalii kwani zimekuwa zikionesha uhalisia wa utaduni wa watu wa Bali.Akiwa amefuatana na Mama Mwanamwema Shein pamoja na ujumbe wake Rais Dk. Shein alijionea jinsi ya eneo hilo lilivyosanifiwa kwa mapambo mbali mbali ambayo yanaonesha uhalisia na alama ya watu wa Bali ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kujionea ngoma na nyimbo za utamaduni wa kisiwa hicho zilizotumbuizwa na kikundi maalum. Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alitembelea eneo maalum la utamaduni ambalo limekuwa likitoa fursa kwa watu mbali mbali wa Bali kuonesha utamaduni wao kwa kutengeneza vifaa mbali mbali vya kihistoria. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurejea nchini hapo kesho Jumatatu ya tarehe 6 Agosti, 2018.Katika ziara yake hiyo nchini Indonesia Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein pamoja na Mawaziri na watendaji wengine wa Serikali.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo