Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Wazazi na Walezi Watakiwa Kutowa Ushirikiano na Serikali Katika Vitendo Vya Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano na Serikali kuhakikisha vitendo vya uzalilishaji vinaondoka nchini . Hayo alisema leo huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo wakati wa mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya wananchi dhidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto ulioandaliwa na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto.. Alisema serikali imetunga sheria kwa wale wote wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto lakini kila siku vitendo vinaendelea hivyo iko haja ya mashirikiano ya pamoja kati ya walezi wazazi na serikali ili kuvidhibiti vitendo hivyo . Aidha alisema tupange mikakati madhubuti kwa pamoja jinsi ya kuondoa wimbi sugu la udhalilishaji wanawake na watoto na hata watu wazima na kuhakikisha kila mmoja anahusika katika mapambano ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia .. Nae mshiriki wa mdahalo huu Shadida Machano alisema wazazi wawe karibu na watoto wao na kuwalea malezi ya kirafiki ambayo yanazingatia maadili ili kumjengea mtoto uwezo wa kusema kwa kila ambalo linamtokezea . Alisema skuli ziandaliwe masomo maalumu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari ili kuweza kujielewa na kujihami. Hata hivyo alisema ingawa jamii imeharibika kwa kiasi kikubwa kutokana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hivyo iko haja walimu wa skuli pamoja na madrasa kupewa mafunzo maalumu. Nae mshiriki wa mdahalo huo kheir Miraji othmani wa Chukwani alitoa rai ya nini kifanyike ili kudhibiti vitendo hivi alisema itolewe adhabu ya mara moja uliyo madhubuti kwa haraka . “Amekutwa pale pale avuliwe nguo apigwe mikwaju katikati ya umati wa watu, kwani yeye si kadhalilisha basi adhalilishe,afungwe kifungo ch maisha. “ alisema kheir Miraji mmoja wa wazazi. Bi Raya Mohamed Sleiman wa Mchangani alieleza hali halisi ya kukosa mashirikiano kwa polisi na mahakama jambo ambalo linavunja moyo na kurejesha nyuma juhudi za kupiga vita vitendo hivyo. “Tatizo hatuna nia ya dhati kuliondoa hili jambo kwa sababu kwa nini tunalindana? udhalilishaji imekuwa kama biashara ya kujiingizi fedha kwa njia ya ruchwa hivi kweli muhalifu anatoroka kituoni “alisema bi Raya. Alisema sheria zinaachwa katika makaratasi hazitekelezwa hii inaonyesha wazi huu ni mtandao maalum ambao kama serikali ipo tayari kuuvunja unaweza kwani ushahidi umeonyesha imepiga vita mifuko ya plastic imeweza helment imeweza na hili haishindwi . Nae Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico alitoa wito kwa wazazi na walezi kuvuata maadili katika malezi na makuzi ya watoto ili kujenga maandalizi mema kwa ajili ya taifa la kesho. Nae Jaji Mshebe Ali Bakari alieleza suala la kuporomoka kwa maadili kwa vijana na watoto kunachangia kuimarisha vitendo vya udhalilishaji hivyo iko haja ya wazazi na walezi kurekebisha maadili ilI kuzuia udhalilishaji kwa pamoja Baina ya wazazi na serikali
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo