Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Azungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kichina ya Futang Group Limited
Kampuni ya Kimataifa ya utengenezaji wa Mipira ya Gari ya Futang Group Limited kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China imeonyesha nia ya kutaka kujenga kiwanda cha Kutengeneza Matairi ya Gari, Baskeli na vyombo vyengine vya Maringi Mawili Visiwani Zanzibar ili kulihudumia soko la Tanzania pamoja na Ukanda wa Afrika Mashariki. Uamuzi wa Kampuni hiyo umekuja Wiki moja tu baada ya Tanzania kutangaza fursa wa Uwekezaji ilizonazo katika Maonyesho ya 15 ya Kimataifa ya Biashara ya China - Asean Expo 2018 yaliyofanyika wiki iliyopita katika Mji wa Nanning ndani ya Jimbo la Guangxi Nchini China. Nia ya kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Futang Group Limited Bwana Tang Biao aliyeuongoza Ujumbe wa Viongozi Watatu wa Kampuni hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. Bwana Tang alisema Kiwanda cha Kampuni hiyo kimeshapata uzoefu wa kutengeneza matairi ya Vyombo vya usafiri katika mazingira ya kutopata pancha hata iwapo mipiRa hiyo itapambana na misumari mingi zaidi wakati chombo kinapokuwa katika safari zake za kawaida bara barani. Alisema Wataalamu wa Kiwanda hicho tayari wameshayafanyia majaribio matairi yanayozalishwa kwa takriban miaka 13 sasa ambapo mpira hata kama utapata misumari mara 200 bado utakuwa na uwezo wa kutembea bila ya kuleta athari yoyote. Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Futang Group Limited alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Tairi linalozalishwa na Kapuni hiyo lina uwezo wa kutembea katika kipindi cha Miaka Miwili hadi Mitatu hata kwenye kwenye bara bara zisizokuwa katika kiwango. Alieleza kwamba Uongozi wa Kampuni yake uko tayari kutoa mualiko kwa Wataalamu wa ufundi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenda kuangalia harakati za uzalishaji za kiwanda hicho kwa lengo la kujiridhisha kutokana na umakini wa Bidhaa zake. Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umekuja na Habari njema yenye nia ya kutaka kulitumia Soko la Tanzania katika Uwekezaji wa Viwanda vyao. Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa msaada wowote utaohitajika kwa Uongozi wa Kampuni hiyo katika azma yake ya kutaka kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar ambayo kwa umuhimu wake itasaidia kutoa huduma ndani ya Soko la Afrika Mashariki. Alifahamisha kwamba Sera ya Uwekezaji iliyopo Nchini hutoa punguzo la Kodi kwa Mali Ghafi zinazotolewa Nje ya Nchi kuzipatia Kampuni au Taasisi zitakazoazimia kuanzisha Miradi yao ya Kiuchumi na Biashara hapa Nchini. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo kuandika Maombi na kuyawasilisha kwa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} ili kuchukuliwa hatua zitakazofaa katika kuona malengo ya nia yao yanafanikiwa.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo