Drop Down Menu
FOR VISITORS
Tourism
Work in Zanzibar
Investment
Business
Study in Zanzibar
Immigration

FOR CITIZEN
Travel Documents
Zanzibar ID
National ID
Social Security
Driving Licence
Health System
E-Government
Zanzibar Port
Municipality

Quick Links
Ikulu Zanzibar
Tanzania
Baraza la Wawakilishi
Bunge Tanzania
Zanzibar Electoral Commission
National Electoral Commission

Zanzibar
Zanzibar
Government News Highlights
Balozi Seif akagua ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Askari Polisi kisiwani Pemba
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uamuzi wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania wa kujitafutia Nyumba za Makaazi ya Askari wake ni jambo la msingi litakalosaidia kurejesha Heshima ya Jeshi hilo. Alisema kitendo cha Askari kuishi Mitaani pamoja na Raia kwa kiasi kikubwa kinapunguza uwajibikaji wa walinzi hao kunakosababishwa na ukaribu unaochangia kushindwa kumchukulia hatua jirani au Jamaa anayekuwa naye pamoja Askari husika kwa muda mwingi. Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofganya ziara fupi ya kuukagua mradi wa ujenzi wa Nyuumba za Makaazi za Jeshi la Polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya Jeshi hilo iliyopo katika Mtaa wa Mfikiwa Chake Chake Kisiwani Pemba. Alisema raia anapofanya makosa katika mazingira anayoishi pamoja na Askari Polisi, mlinzi huyo anakuwa mzito kumchukulia hatua za kisheria Raia huyo jambo ambalo hupunguza nidhamu ya kazi ya Ulinzi. Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa hatua uliofikia wa kufikia maamuzi ya kuwatafutia stara wapiganaji wake ili kuwapunguzi hofu wanapokuwa Mitaani hasa pale wanapowachukulia hatua za kisheria Wananchi wanaoishi nao Mitaani. “ Mimi mwenyewe wakati wote ninapokutana naViongozi wenu wa ngazi ya Juu kama IGP nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa Jeshi la Polisi kuwa na nyumba zao za Makaazi ili kupunguza maisha ya uraiani yanayochangia uzoroteshji wa majukumu ya Jeshi hilo”. Alisisitiza Balozi Seif. Alisema Seikali zote mbili Nchini Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zilikuwa na wakati mgumu wa kufikiria kulitafutia ufumbuzi tatizo la Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi Nchini lililokuwa kero kwa muda mrefu. Mapema akitoa Taarifa ya ujenzi wa Mradi huo wa Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi Mikoa Miwilio Kisiwani Pemba Kamanda wa Polisi Mkoa Kusini Pemba Kamishna Msaidizi wa Polisi Said Omar Dadi alisema mradi huo ulianzishwa maalum kwa lengo la kupunguza ifunyu wa Nyumba za Makaazi ya Askari. Kamishna Msaidia wa Polisi Said alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo unaendelea vyema kwa ujenzi wa Nyumba Sita Awamu ya kwanza zitakazokuwa na uwezo wa kuishi Familia 24. Kamanda huo wa Polisi Mkoa Kusini Pemba kwa niaba ya Askari wa Jeshi hilo Kjisiwani Pemba amewashukuru na kuwapongeza Viongozi wa Serikalik zote mbili Nchini Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono uendelezaji wa ujenzi wa Nyumba hizo muhimu kwa Jeshi la Polisi. Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullah alisema Uongozi wa Mkoa huo pamoja na Wananchi wataendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuona Mradi huo unafanikiwa kama ulivyokusudiwa. Mh. Hemed alisema ushirikiano huo umejitokeza pale mradi huo ulipokumbwa na changamoto ya upatikanaji wa rasilmali ya Mchanga ambayo Mkoa ukatumia busara zake katika kuitafutia dawa Changamoto hiyo.
Official Reports
MUONGOZO WA KUOMBA KIBALI CHA UTAFITI-Date Posted: 17-09-2018
FOURTH SCHEDULE (KIAMBATANISHO)-Date Posted: 17-09-2018
RESEARCH/FILMING APPLICATION FORM -Date Posted: 17-09-2018
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED KUHUSU MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 -Date Posted: 25-07-2018
RATIBA YA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI UTAKAOJADILI BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019-Date Posted: 10-05-2018

Research

Procedure
Research in Zanzibar
Publications
Conferences
PROJECTS

Ongoing Projects
Upcomming Projects
Previous Projects
Reports in Projects
Publication from Projects
GALLERY

Government Activies
Kilimo