Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

Image

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi ilianzishwa mwaka 2018 kutokana na mabadiliko yaliofanywa na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu namba 42(1) toleo la 2010 na kukabidhiwa  majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kwa maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.

  • Kutayarisha, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Miongozo inayohusu Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.
  • Kusimamia Rasilimali Ardhi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
  • Kuwezesha Kuwepo kwa uwiano wa matumizi ya ardhi kwa ajili ya Shughuli za Kiuchumi na Kijamii Zanzibar.
  • Kuratibu Mpango wa Maendeleo katika vijiji kwa ajili ya kukuza utalii.
  • Kuhakikisha upatikanaji wa Makaazi bora kwa Wananchi Mijini na vijijini.
  • Kuhifadhi na kuendeleza Mji Mkongwe wa Zanzibar kama ni Urithi wa Dunia.
  • Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote.
  • Kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Nishati ilio Salama na endelevu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
  • Kufanya mawasiliano na Taasisi zote zilizochini ya Wizara na Sekta nyengine ndani na nje ya Nchi.
  • Kufuatilia na Kutathmini Miradi ya Maendeleo iliochini ya Wizara.


    Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
    S.L.P 238
    Simu: +255 242941193

    Barua pepe : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Mhe. Riziki Pembe Juma

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Mhe. Riziki Pembe Juma. 

Angalia Taarifa Binafsi

Tovuti

http://www.ardhismz.go.tz

Pitia Tovuti