Biashara na Viwanda

Image
Biashara, viwanda na masoko ni muhimu katika maendeleo ya uchumi. Sekta ya biashara ni muhimu katika kuinua viwango vya maisha, kutoa ajira na kuwezesha raia kupata  bidhaa mbalimbali.
Kipengele hiki kitakupa taarifa zinazohusiana na sera, fursa za masoko, viwango na kanuni, bima,  utaratibu wa usajili wa biashara ndogo na za kati pamoja na kupata leseni za katika kukuza biashara nchini wizara iliundwa na idara ya Biashara biashara na ukuzaji masoko ni miongoni mwa idara mama zilizo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar. 
Idara hii ni inaongozwa na sheria ya biashara ya nam 14 ya mwaka 2013 “The Zanzibar Trading Act No 14 of 2013”. 
Idara hii kwa ujumla wake husimamia na kutekeleza sheria na sera zinazohusiana nabiashara Zanzibar 
pamoja na kuhamasisha (kukuza) masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
 
Idara imeweza kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha inaimarisha hali ya biashara Zanzibar. 
Kumekuwa na ongezeko la bidhaa zinaoingia ndani ya nchi na kuongezeka kwa thamani kwa asilimia 68 
kutoka bidhaa zenye thamani ya TZS bilioni 211.42 mwaka 2017 na kufikia TZS bilioni 355.85 mwaka 2018 
huku mazingira ya kufanya biashara yamewekwa kuwa rafiki kwa waekezaji nchini.
 

Mhe. Omar Said Shaaban
Waziri wa Biashara, na Maendeleo ya Viwanda.

Mhe. Omar Said Shaaban

Angalia Taarifa Binafsi

Tovuti

https://tradesmz.go.tz

Pitia Tovuti