Elimu

Image

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kutambua umuhimu  wa elimu ilitangaza elimu ya msingi bure kwa Wazanzibari wote, kwa kupanga mipango ya muda mfupi na mrefu ya kupata elimu bora kwa Wazanzibari wengi bila ya kujali makabila, dini au jinsia. Mnamo mwaka 2006 Serikali iliidhinisha sera ya elimu kwa lengo la kuongeza utoaji wa elimu bora ambayo ni pamoja na miaka miwili ya masomo ya awali, miaka sita ya kiwango cha msingi na miaka minne ya sekondari.
kipengele hiki kinatoa maelezo kuhusu sera za elimu, sheria, kanuni na miongozo pamoja na huduma za elimu.


 

 1. Kuratibu na kutayarisha Mitaaala ya Elimu.
 2. Kutoa miongozo ya kufundishia na kujifunzia.
 3. Kupanga na kutoa viwango vya ufaulu wa Elimu.
 4. Kusimamia maendeleo ya Elimu.
 5. Kusimamia, kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo ya Elimu.
 6. Kutoa miongozo ya Elimu maalumu.
 7. Kuandaa Sera ya Elimu.Kutoa miongozo ya uanzishaji wa Skuli binafsi na jamii.
 8. Kusajili Skuli za binafsi, Skuli za jamii na vituo vya kujiendeleza.
 9. Kushughulikia maombi na kutoa leseni za walimu za kufundishia.
 10. Kutoa miongozo kuhusu uhamisho wa wanafunzi.
 11. Kuandaa Mitihani ya Taifa kwa ngazi ya msingi, sekondari na vyuo vya ualimu.
 12. Kusimamia na kuweka uwiano baina ya walimu na wanafunzi.
 13. Kutoa miongozo ya uongozi na utawala katika skuli, vituo na vyuo vya ualimu.
 14. Kushughulikia madai ya maslahi ya wafanyakazi.
 15. Kuwapangia kazi watumishi wa Wizara kwa mujibu wa mahitaji.
 16. Kuratibu huduma za TEHAMA katika Elimu.
 17. Kutoa na kusimamia mafunzo ya watumishi.
 18. Kutoa na kusimamia mafunzo ya ualimu.
 19. Kusimamia ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
 20. Kuratibu ajira, kuthibitisha na kupandisha cheo watumishi.
 21. Kukamilisha majengo ya skuli yaliyoanzishwa na wananchi.
 22. Kuratibu na Kusimamia shughuli za Michezo na sanaa. 
 • AJESR - Tathmini ya pamoja ya sekta ya Elimu 2020 (AJESR 2020) 9 - 11 Machi, 2020
 • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

  P.O.Box 394,
  MAZIZINI-ZANZIBAR
  Zanzibar, United Republic of Tanzania

 • E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 • Telephone: +255 24 223 2827

 • Fax: +255 24 223 2827
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali

Mh. Simai Mohamed Said

Angalia Taarifa Binafsi

Website

www.moez.go.tz   

Pitia Tovuti