Hayati: Sheikh Abeid Amani Karume
Rais wa Awamu ya kwanza wa Zanzibar.
Awamu ya Kwanza ya Uongozi wa Kitaifa Zanzibar ilikuwa chini ya Chama cha Afro-Shirazi kilichoongozwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambaye alikuwa ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Awamu hii ni muhimu sana katika historia ya nchi ya Zanzibar. Ndiyo Awamu iliyoweka dira ya mwelekeo wa Zanzibar katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ili kufikia malengo yaliyowekwa na Chama cha Afro Shirazi Party (ASP). Ni dhahiri kwamba awamu hii ililazimika kuchukua hatua madhubuti na kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa lengo la Mapinduzi linafikiwa na kuwanufaisha Wazanzibari wote. Uongozi ulifuata misingi ya kuongozi kwa kuonesha njia ambapo viongozi wa Serikali walikuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa kila shughuli ya maendeleo iliyofanywa na wananchi. Hiki ni kipindi ambacho dhana ya kujitolea katika ujenzi wa Taifa ilikuwa ndio dira ya utekelezaji wa shughuli za Serikali. Katika hali hiyo Serikali ya ASP ilianza kutekeleza ahadi zake zilizoorodheshwa katika Manifesto ya ASP.
7 Aprili, 1972 - 27 Januari, 1984
Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar
31 Januari, 1984 - 17 Oktoba, 1985
Mheshimiwa: Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Awamu ya Tatu wa Zanzibar
Baada ya kujiuzulu Rais wa Awamu ya Pili, kiongozi aliyeteuliwa kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar ni Mzee Ali Hassan Mwinyi. Nafasi ambayo alidumu nayo kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kabla ya kuteuliwa na kuchaguliwa kushika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Mheshimiwa Seif Sharif Hamad kushika nafasi ya Waziri Kiongozi ambaye, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, alikuwa ni msaidizi wa Rais na Mkuu wa shughuli za Serikali katika Baraza la Wawakilishi
17 Oktoba 1985 - 25 Oktoba, 1990
Hayati: Mzee Idris Abdulwakil
Rais Awamu ya Nne wa Zanzibar
Halmashauri Kuu ya CCM ilipitisha jina la Mhe. Idris Abdulwakil kwa ajili ya uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Oktoba, 1985. Mzee Idris Abdulwakil naye aliendeleza mfumo ule ule wa Serikali wenye kuzingatia mihimili mitatu ya Dola ambapo pia alimteua Mhe. Seif Sharif Hamad kuendelea na wadhifa wa Waziri Kiongozi. Hata hivyo, katika kuimarisha utendaji wa Serikali, tarehe 26 Januari 1988, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alilivunja Baraza la Mapinduzi na baadae kumteua Mheshimiwa Dkt. Omar Ali Juma kushika nafasi ya Waziri Kiongozi badala ya Mhe. Seif Sharif Hamad. Uongozi wa Mheshimiwa Idris Abdulwakil ulimalizika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 1990.
25 Oktoba, 1990 - 8 Novemba, 2000
Mheshimiwa Dkt. Salmin Amour Juma
Rais wa Awamu ya Tano wa Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Tano iliongozwa na Dkt. Salmin Amour Juma na ilifuata mfumo wa uongozi sawa na wa Awamu zilizotangulia. Hata hivyo, Awamu hii ilikuwa na mabadiliko makubwa katika safu za siasa na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Awamu ya tano ilikuwa ni ya vipindi viwili kisiasa. Kipindi cha kwanza cha uongozi kilianza (1990-1995) na muendelezo wa mfumo wa utawala wa Chama kimoja cha siasa hadi mwaka 1992 ambapo mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa tena. Katika uongozi wa miaka 10 wa Rais Dkt. Salmin Amour Juma, Serikali ilitilia mkazo kuimarisha uchumi na mawasiliano ya kisiasa.
Katika kipindi cha kwanza cha uongozi Dkt. Omar Ali Juma aliteuliwa kuwa Waziri Kiongozi na katika kipindi cha pili alimteuwa Dkt. Mohamed Gharib Bilali kuwa Waziri Kiongozi. Aidha katika kipindi hichi ilianzishwa nafasi ya Naibu Waziri Kiongozi ambapo Mhe. Omar Ramadhan Mapuri aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Kiongozi. Kipindi hiki cha uongozi baada ya Uchaguzi Mkuu chini ya mfumo wa vyama vingi kilikuwa kigumu kutokana na kususiwa misaada na wafadhili wa nje, hasa kutoka nchi za magharibi kutokana na sababu za kisiasa.
8 Novemba, 2000 - 3 Novemba, 2010
Mheshimiwa: Dkt. Amani Abied Karume
Rais wa Awamu ya sita wa Zanzibar.
Serikali ya awamu ya sita iliongozwa na Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume baada ya kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2000 na 2005. Awamu ya sita ya uongozi ilikuwa na vipindi viwili (2000-2005) na (2005-2010). Kama awamu zilizopita Serikali ya Awamu hii iliendelea kulinda na kuendeleza misingi iliyowekwa. Katika vipindi vyote hivyo Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume alimteuwa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kuwa Waziri Kiongozi. Na katika kipindi cha pili alimteuwa Mhe. Ali Juma Shamuhuna kuwa Naibu Waziri Kiongozi.
Mabadiliko hayo ya Katiba yalitokana na maamuzi ya viongozi wa vyama vya siasa (Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Mhe. Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu Civil United Front (CUF) Taifa ya kukubali kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Maamuzi ya viongozi hawa yaliungwa mkono na wananchi wa Zanzibar katika kura ya maoni iliyopigwa tarehe 31 Julai, 2010. Uongozi wa Dkt. Amani Abeid Karume ulimazika baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
3 Novemba, 2010 - 3 Novemba 2020
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein
Rais wa Awamu ya Saba wa Zanzibar
Katika Awamu ya Saba ya Urais wa Zanzibar chini ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umebadilika kutoka mfumo wa Serikali inayoongozwa na Chama kilichoshinda peke yake kwenda katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo chama kilichoshinda kinashirikiana na chama kilichoshika nafasi ya pili katika kuunda Serikali.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaongozwa na Rais ambaye anasaidiwa na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais na kufuta nafasi ya Waziri Kiongozi iliyokuwepo kabla ya marekebisho hayo ya Katiba. Kwa mujibu wa marekebisho hayo, Rais anatoka Chama kilichoongoza katika Uchaguzi Mkuu, Makamu wa kwanza wa Rais anateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Chama kilichoshinda nafasi ya pili katika matokeo ya uchaguzi wa Rais; na Makamu wa Pili wa Rais anateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama anachotoka Rais na ndiye atakayekuwa Mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali. Marekebisho hayo pia yamemuweka Katibu wa Baraza la Mapinduzi kuwa ni Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Zanzibar.
Aidha, muundo huu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Mfumo wa Umoja wa Kitaifa umeendelea kuendesha shughuli zake kupitia Baraza la Wawakilishi ambacho ndicho chombo kikuu cha kutunga Sheria Zanzibar, Baraza la Mapinduzi pamoja na Mahakama. Mihimili yoye mitatu inafanya kazi kwa uhuru na kujitegemea. Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaendelea kulinda na kutetea malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka1964 kwa kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kuwa kitu kimoja na kusahau tafauti zao za kisiasa.
3 Novemba, 2020 - Mpaka Sasa
Rais wa Awamu ya Nane wa Zanzibar
kutoa Taarifa kwa Jamii kuhusu shughuli zinazotekelezwa na taasisi za Serikali.