Mawasiliano na Usafirishaji

Image
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji (WUMU) ilianzishwa mwezi April, 2016 baada ya uchaguzi mkuu na kuchukua nafasi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya zamani.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ilianza kipindi cha ukoloni wakati huo ikijulikana kama Idara ya Ujenzi wa Umma ikiwa imepangiwa majukumu ya kusimamia huduma za umma, ikiwa ni pamoja na kazi, barabara, umeme, maji na makazi. Mwaka 1964, ilikuwa imegawanywa katika wizara mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi, Barabara na Nishati na Wizara ya Maji na Makazi.
Mwanzoni mwa mwaka 1970 Wizara ya Ujenzi, Barabara, na Nishati ikawa Wizara ya Ujenzi, Barabara na Mawasiliano wakati sehemu ya mawasiliano ya simu iliongezwa na kifungu cha nishati ikiongozwa na wizara nyingine. Katika miaka ya 1970 ilibadilishwa na kuwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ikiwa na jukumu la kusimamia maendeleo na udhibiti wa usafiri na mawasiliano.kipengele hiki kinaeleza kuhusu huduma, sera, kanuni na miongozo inayohusiana na usafirishaji, mawasiliano na ujenzi.

 • Kuridhisha wateja katika utoaji wa huduma.

 • Kuhakikisha usalama katika mfumo wa usafiri.

 • Kuhakikisha upatikanaji wa huduma za usafiri zilizobora, endelevu na zenye kuaminika.

 • Kuboresha uwezo wa taasisi katika kutoa huduma kwa ufanisi.

 • Kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu ya usafiri na mawasiliano iyobora, salama na yenye kufanyakazi.

 • Kutoa elimu ya maambukizo ya virusi vya ukimwi kwa watumishi na wadau katika sekta ya usafiri na mawasiliano.

 • Kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa taasisi zote.

 • Kuinginza masuala ya jinsia katika sekta ya usafiri na mawasiliano.

 • Zanzibar ICT Policy
 • Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji
  P.O.Box 266
  ZANZIBAR
  TANZANIA
 • 190 FUMBA ROAD
  POSTCODE: 71201
  ZANZIBAR, TANZANIA

 • email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


Mhe. rahma Kassim Ali
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Mhe. Rahma Kassim Ali.

Angalia Taarifa Binafsi

Tovuti

https://www.moic.go.tz

Pitia Tovuti