Jamii na Usalama

Image

Uwajibikaji wa mfumo wa Serikali ni kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa watu kwa ushirikiano mzuri katika ngazi mbali mbali. Sekta hii inajukumu la kulinda usalama wa ndani, kuzuia usafirishaji wa bidhaa za magendo pamoja na huduma zote zinazomuhusisha mwananchi kamavile vitambulisho vya mzanzibar.

Kipengele hiki kinaelezea huduma, sera, kanuni na miongozo ya upataji wa huduma zilizopo kwenye sekta hiyo
 • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ina majukumu makuu yafuatayo:-

  • Kusimamia Sera, Sheria na Kanuni mbali mbali za Ofisi.
  • Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
  • Kudumisha Amani, Ulinzi na Usalama katika Mikoa na Wilaya hadi Shehia.
  • Kulinda mali za Taifa na za watu binafsi zisiharibiwe, kuzuia uingizaji au utoaji nje ya nchi kimagendo, pamoja na kusimamia kazi za uzimaji moto na uokozi.
  • Kuwasajili na kuwapa vitambulisho Wazanzibari wakaazi.
  • Kuwahifadhi kwa kufuata taratibu bora na kwa kuzingatia haki za binaadamu watuhumiwa na waliofungwa ambao wako katika Vyuo vya Mafunzo.
  • Kuandaa na kutekeleza mipango ya kuijengea uwezo Mikoa kitaaluma na utumishi katika Mikoa.
  • Kutoa mwongozo na ushauri kwa Mikoa katika mambo ya kisheria na utaratibu, kujenga mazingira mazuri katika kuimarisha huduma za kijamii na kiuchumi katika Mikoa.
  • Kuratibu, kushauri, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuliza Serikali za Mitaa.
  • Kuimarisha Utawala Bora na kuimarisha uwezo wa Serikali za Mitaa na mamlaka zake.
  • Kufuatilia na kukagua utendaji wa mamlaka za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika utoaji wa huduma.
  • Kuendeleza michezo katika Idara na Taasisi zetu.
  • Kuimarisha uhusiano baina ya taasisi za Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ. 
 • Application of Zanzibar National ID
 • Bussiness Registration
 • Birth Certificate
 • Guiding Principal
 • Policy for Local Governace 
 • S.L.P 4220               
  Vuga - Zanzibar
  Simu: +255242230034
  Nukshi: +255242230034
  Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mhe. Masoud Ali

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.

Mhe. Masoud Ali Mohammed

Angalia Taarifa Binafsi

Tovutii

www.tamisemim.go.tz

Pitia Tovuti