Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale

Image

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa mwaka 2020, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Mheshimiwa Rais
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu 42 (1) cha Katiba ya mwaka 1984, na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Utalii na Mambo ya Kale.
 

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa kutokana na shughuli zake kufanana
na kutegemeana katika utendaji wa kazi.Hivyo,kuziweka katika Wizara moja shughuli hizo kutasaidiakupatikana ufanisi, kusukuma kasi ya maendeleo na kuimarisha uchumi.
 Wizara inashughulikia Sekta 
kuu mbili (2) za Utalii na Mambo ya Kale. 
Sekta ya Utalii inajumuisha Kamisheni ya Utalii na Idara ya Utalii. Taasisi hizi zimekabidhiwa jukumu la kupanga,
kusimamia, kuendeleza Utaliina   kuitangaza Zanzibar kama ni kivutio Zanzibar  cha utalii ili kwenda sambamba  na sera, mikakakti na Dira ya Taifa katika kufikia Malengo makuu ya kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini.
 Kwa upande wa Mambo ya Kale, Sekta inaundwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale.
Sekta hii imekabidhiwa jukumu la kuhifadhi, kuimarisha na kutunza maeneo na vitu vya kale na kihistoria
ili visaidie katika kuimarisha uchumi na kutunza historia kwa vizazi vijavyo.
 

  • Kusimamia na kuendeleza Utalii kwa lengo la kuinua pato la Taifa na uchumi wa wananchi.
  • Kutangaza utalii ndani na nje ya nchi.
  • Kuhifadhi, kulinda na kuendeleza maeneo yote ya kihistoria nchini.
  • Kukusanya mapato ya huduma zinazotolewa katika Maeneo ya Kihistoria na Kamisheni ya Utalii.
  • Kuratibu uibuaji wa miradi, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia sekta ya Utalii na Mambo ya Kale.
  • Kuandaa Sera, Sheria na mikakati ya kuendeleza sekta ya Utalii na Mambo ya Kale pamoja na kusimamia utekelezaji wake.

PDF DOCS 

HOTUBA_BAJETI_20212022_WIZARA_YA-UTALII.pdf 

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz

Hon. Mahmoud Thabit Kombo
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale

Mhe. Leila Mohammed Mussa
 View Profile
http://www.utaliismz.go.tz

Website

View Website