Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba
pamoja na Visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

kwa ujumla visiwa hivi vipo baina ya latitude na Digrii 6 kusini mwa mstari wa Ikweta na longitudi 39.55 na Digrii 40 Mashariki, Zainzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zanzibar ina Miongo 4 ya majira ya hali ya hewa katika mwaka wa Kalenda inayoanzia mwezi wa Januari hadi Disemba ambayo inahusisha majira ya Kaskazi (Disemba hadi Febuari), Masika (Machi hadi Mei), Kipupwe (Juni hadi Septemba) na Vuli (Oktoba hadi Novemba). 

Mikoa ya Zanzibar
Zanzibar ina jumla ya Mikoa 5, kati ya hiyo, Mikoa 3 ipo katika Kisiwa cha Unguja ambayo ni Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja na Mikoa 2 ipo katika Kisiwa cha Pemba ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika kuwasogezea wananchi huduma za kiutawala katika maeneo yao, jumla ya Wilaya 11 zilianzishwa ambazo ni: Wilaya ya 
Mjini, Wilaya ya Magharibi A, Wilaya ya Magharibi B, Wilaya ya Kusini, Wilaya ya Kati, Wilaya ya Kaskazini A, Wilaya ya Kaskazini B, Wilaya ya Chake Chake, Wilaya ya Mkoani, Wilaya ya Wete na Wilaya ya Micheweni, ambapo jumla ya Shehia 388 zimeanzishwa ndani ya Wilaya hizo. Zanzibar ina eneo la maili 637 za mraba.